Willian arudi Brazil mkewe, mtoto waugua corona

Wednesday March 25 2020

Willian arudi Brazil mkewe, mtoto waugua corona ,Chelsea ,maambukizi ya ugonjwa wa corona,

 

London, England. Chelsea imetoa ruksa kwa winga wake Willian kurejea Brazil kumuona mkewe na mwanaye waliopata maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Winga huyo aliomba ruksa ya kurejea nyumbani kuungana na familia yake ambayo imekumbwa na janga hilo.

Ugonjwa wa corona umesababisha michezo yote kusitishwa duniani ili kuepuka mkusanyiko wa watu.

Hata hivyo, haijafahamika mchezaji huyo atakuwa Brazil kwa muda gani kwa kuwa itategemea na hali ya usalama itakavyokuwa hapo baadaye.

Winga huyo amepata baraka hizo wakati kukiwa na agizo kuwa watu watakuwa chini ya ungalizi maalamu Uingereza.

Ligi Kuu England imesogezwa mbele hadi Aprili 30 kulingana na hali itakavyokuwa.

Advertisement

Willian mwenye miaka 30, amedumu Chelsea inayonolewa na kiungo wake wa zamani Frank Lampard kwa miaka saba.

Advertisement