Wapinzani Stars watangaza vikosi

Muktasari:

Tanzania imepangwa katika kundi J sambamba na timu za Tunisia, Guinea ya Ikweta na Libya ambapo nchi mbili zitakazoongoza kundi hilo zitashiriki Fainali za Afcon

WAKATI timu ya taifa, Taifa Stars ikiingia kambini leo Jumamosi, wapinzani wao kwenye Kundi J katika kuwania Fainali za Afrika (Afcon) 2021, Tunisia na Guinea ya Ikweta zimetangaza vikosi vyao kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao itakayochezwa wiki ijayo.


Kocha wa Guinea ya Ikweta, Sebastien Migne ametangaza kikosi cha nyota 26, huku kundi kubwa likiwa ni wale wanaocheza soka la kulipwa nje ya bara la Afrika, kwa ajili ya mchezo wa kufungua dimba dhidi ya Tanzania ugenini mnamo Novemba 15 na baada ya hapo itakuwa nyumbani kuialika Tunisia, Novemba 19.


Nyota wa zamani wa Birmingham City, Middlesbrough na Real Mallorca, Emilio Nsue anatarajiwa kuongoza kikosi hicho ambacho pia kinamjumuisha nyota wa Real Zaragoza, Federico Akieme.


Kikosi kamili cha Guinea ya Ikweta kinaundwa na makipa Felipe Ovono, Aitor Gil na Jesus Owono wakati mabeki ni Luis Alberto Meseguer, Marvin Jose, Jorge Ramon Akapo, Miguel Nzang, Igor Noval, Vicente Esono, Esteban Orozco, Carlos Akapo Martinez na Basilio Ndong Owono.


Viungo wanaounda kikosi hicho ni Ruben Belima Rodrigues, Pablo Ganet Comitre, Yannick Buyla Sam, Nicolas Kata, Pedro Mba Obiang, Jose Machin Dicimbo na Federico Bikoro Akieme wakati washambuliaji ni Joan Lopez Elo, Ivan Salvador Edu, Jose Antonio Miranda, Emilio Nsue, Pedro Oba Asu, Enrique Boula Senobua na Jordan Gutierrez Nsang.


Kwa upande wa Tunisia ambayo itakabiliana na Libya na baadaye Guinea ya Ikweta, kocha mkuu wa timu hiyo Mondher Kebaier ametangaza kikosi cha wachezaji 25 ambapo kati ya hao, sita wanacheza soka katika klabu za ndani nchini humo.


Baada ya kukosa Fainali za Afcon 2019 zilizofanyika Misri, beki wa Al Ahly, Ali Maâloul amerejeshwa kikosini kama ilivyo kwa kiungo mshambuliaji Youssef Msakni wa Al Duhail ya Qatar.


Kikosi hicho kinaundwa na makipa Farouk Ben Mustapha (Al Shabab), Moez Hassan (Nice) na Moez Ben Cherifia (Esperance Tunis) wakati mabeki ni Aymen Abdennour (Kayserispor), Dylan Bronne (KAA Gent), Yassine Meriah (Olympiacos), Ayman Ben Mohamed (Le Havre), Mohamed Drager (Paderbon), Saddam Ben Aziza (Etoile du Sahel), Ali Maâloul (Al Ahly), Wajdi Kechrida (Etoile du Sahel), Hamdi Nagguez (Zamalek) na Oussama Haddadi (Al Ettifaq).


Viungo ni Anice Badri (Etoile du Sahel), Ghaylen Chaalali (Malatyaspor), Naim Sliti (Al Ettifaq), Youssef Msakni (Al Duhail), Hamza Rafia (Juventus), Saad Bguir (Al Abha), Elyes Skhiri (FC Cologne), Ferjani Sassi (Zamalek), Seifeddine Khaoui (Marseille) na Mohamed Ben Romdhane (Etoile du Sahel) wakati washambuliaji ni Wahbi Khazri (Saint Etienne) na Yassine Khenissi (Etoile Du Sahel).