Waalgeria wameanza ng’ebe eti! Taifa Stars ni kidole kidogo cha mwisho katika Kundi C

Monday April 15 2019

 

Alger’s, Algeria. Timu Tanzania ipo nafasi 131 katika orodha ya viwango vya Fifa ikiwa Kundi C pamoja na Algeria, Kenya na Senegal.

Taifa Stars imefuzu kwa mara ya pili kwa fainali za Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kwao baada ya miaka karibu 40.

Tangu ilipofanya hivyo 1980 nchini Nigeria. Haikuweza kufuzu tena kwa mashindano hayo makubwa Afrika hadi mwaka huu.

Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Emmanuel Amunike atakuwa akijaribu japo kuvuka kwa raundi ya 16 bora, hasa katika fainali hizo za 32 zilizoshirikisha timu 24 kwa mara ya kwanza, hivyo kutoa nafasi timu mbili za kwanza za kila kundi, pamoja na timu nne zitakazomaliza  mshindi wa tatu bora kufuzu kwa hatua ya 1/8.

Hali ya Kundi C inatawaliwa na Senegal na Algeria. Tanzania zitashindana na Kenya kuwania nafasi ya tatu. Timu ya Tanzania inaundwa na wachezaji kadhaa wanaocheza soka nje hasa barani Ulaya na Afrika.

Nyota wa timu hiyo ni mshambuliaji Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk (Ubelgiji). Tanzania pia na wachezaji wengine wanaocheza Ulaya wakiwemo Shaban Chilunda na Farid Musa (Tenerife, Hispania).

Advertisement

Wachezaji wengine wa Tanzania wanaocheza soka barani Afrika katika nchi za Morocco, Misri, Algeria yupo nyota mmoja anayecheza JS Saoura, Thomas Ulimwengu.

Pia, Taifa Star ina wachezaji wanaocheza Botswana na Zambia. Hata hivyo inajulikana nusu ya wachezaji wa Tanzania wanatoka katika kikosi cha Simba mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo.

Hata hivyo katika historia ya mechi za mashindano dhidi ya Tanzania (Kufuzu kwa Afcon, kufuzu Kombe la Dunia na mechi za kirafiki), Algeria imefanikiwa kushinda mechi tatu na kutoka sare tatu na kufungwa mechi moja.

Katika mechi za kufuzu Tanzania imemaliza nafasi ya pili katika Kundi L ikiwa nyuma ya Uganda, huku Tanzania ikishinda mechi mbili.

Advertisement