Vyuma 50 mguu ndani, mguu nje!

Muktasari:

Sambamba na Messi, unaambiwa hivi kunan orodha ya mastaa wakuwa kwenye soka wasiopungua 50 ambao wanaweza kubadili timu zao wanazozitumikia kwa sasa itakapofika mwisho wa msimu na dirisha la usajili litakapofunguliwa. Hii hapa orodha ya mastaa wanaoweza kubadili timu mwisho wa msimu.

LONDON, ENGLAND . DIRISHA la usajili wa Januari limeshapita na kilichotokea kimetokea. Manchester United wamempata mtu wao, Bruno Fernandes na Arsenal wamesajili beki mpya, Pablo Mari.

Lakini, si muda mrefu, miezi michache tu ijayo, dirisha jingine la usajili litafunguliwa. Kwenye dirisha hilo kubwa la usajili wa wachezaji huko Ulaya, mengi yanatarajia kutokea, ikiwamo uvumi wa kwamba supastaa wa Barcelona, Lionel Messi anaweza kuwa mmoja wa mastaa watakaobadili timu kama mambo hayatakuwa mazuri huko Nou Camp.

Hivi karibuni alitibuana na mkurugenzi wa michezo, Eric Abidal na kuzua hofu ya kwamba huenda akaachana na timu hiyo aliyodumu nayo tangu utoto, huku zikitajwa klabu tano zenye uwezo wa kumudu mshahara wake ambazo ni Man United, Manchester City, Juventus, Inter Milan na Paris Saint-Germain.

Sambamba na Messi, unaambiwa hivi kunan orodha ya mastaa wakuwa kwenye soka wasiopungua 50 ambao wanaweza kubadili timu zao wanazozitumikia kwa sasa itakapofika mwisho wa msimu na dirisha la usajili litakapofunguliwa. Hii hapa orodha ya mastaa wanaoweza kubadili timu mwisho wa msimu.

Mario Gotze, Ben Chilwell, Danny Ings, Danny Rose, Jan Vertonghen, Joao Cancelo, Timo Werner, Moussa Dembele, Hwang Hee-chan, Kingsley Coman, Emre Can, Juan Foyth, Layvin Kurzawa, Richarlison, Pierre-Emile Hojbjerg, Thomas Lemar, Isco, Luka Modric, Virgil van Dijk, Olivier Giroud, Mesut Ozil, Boubakary Soumare, Adrian, Jude Bellingham, Cengiz Under, Lionel Messi, Jorginho, Bertrand Traore, Pierre-Emerick Aubameyang, Islam Slimani, Kepa Arrizabalaga, Josh King, Sergio Romero, Jack Grealish, John Stones, Leroy Sane, Christopher Nkunku, Dayot Upamecano, Paul Pogba, Wilfried Zaha, Kai Havertz, Neymar, Kylian Mbappe, Ryan Fraser, Gareth Bale, Jadon Sancho, Kalidou Koulibaly, Willian, Dries Mertens na Edinson Cavani.