VIDEO: Fei Toto akicheza rafu tu, Simba wale...

Muktasari:

Feisal kwa sasa ana kadi mbili za njano akipata nyingine kwenye mchezo huo  na JKT Tanzania mechi yao na Simba itambidi akae juu jukwaani kama shabiki.

Dar es Salaam. Timu ya Yanga itashuka kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga kesho Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania lakini ngoma nzito ipo kwa kiungo wao Feisal Salum.

Yanga ambayo imedhamiria kuvuna alama tatu ili kujiweka  kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu na kuwaacha mbali watani wao Simba.

Timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani hadi sasa ipo kileleni ikiwa na pointi 55, huku wapinzani wao wa kesho JKT Tanzania, wakiwa wamejikusanyia alama 32 katika nafasi ya saba.

Hata hivyo, kiungo wao Feisal Salum ‘Fei Toto"’ yuko kwenye hatihati ya kuikosa mechi ya watani wa jadi Simba iwapo atachezeshwa katika mchezo huo wa kesho na kupata kadi ya njano.

Feisal kwa sasa ana kadi mbili za njano akipata nyingine kwenye mchezo huo  na JKT Tanzania mechi yao na Simba itambidi akae juu jukwaani kama shabiki.