Uganda kufa au kupona kwa Serengeti Boys Afcon

Monday April 15 2019

 

By Thomas Ng’itu

Dar es Salaam. Baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Angola, Kocha mkuu wa timu ya Taifa Uganda chini ya miaka 17, Samuel Kwesi amesema wanataka kushinda mechi yao ijayo dhidi ya Tanzania ili kufufua matumaini yao ya kufuzu kwaFainali za Kombe la Dunia Brazil.

Kocha Kweli alisema matokeo waliyoyapata hajayafurahia, lakini hilo haliwezi kuwakatisha tamaa zaidi ya kuendelea kupambana katika michezo ijayo.

“Tutakaa chini na kuangalia eneo gani ambalo tumekosea ili kubadili hiki ambacho tumekifanya, bado tuna mechi zingine mbele yetu hivyo tunaweza kupata matokeo,” alisema.

Kwasi aliongeza kwa kusifu namna ambavyo wachezaji wake walivyopambana uwanjani, lakini bahati haikuwa katika upande wao kwenye mchezo huo.

Uganda katika mchezo ujao itakutana na Tanzania, mchezo utakaopigwa Jumatano, saa moja usiku katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Advertisement