VIDEO: Tshishimbi: Tumevuna tulichopanda kwa Morrison

Monday July 13 2020

 

By Khatimu Naheka

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema matukio ya kucheza katika kiwango duni kwa mshambuliaji wao Bernard Morrison ni makosa ambayo yametokana na mapungufu ya aina mbili.

Tshishimbi amesema ubora wao mkubwa katika safu yao ya ushambuliaji ulitakiwa kutokana na ubora wa Morrison lakini hakuwa katika ubora.

Tshishimbi amesema Morrison hakuwa sawa kucheza kwa muda mrefu mchezo huo wa jana wa Nusu Fainali ya Kombe la Azam Shirikisho.

"Morrison hakuwa sawa,ukiangalia mchezo wa Kagera kitu pekee bora alichofanya ni kufunga lile bao lakini ukiangalia anavyocheza utagundua hakuwa sawa" amesema Tshishimbi.

"Jana Morrison hakuwa fiti,hakusaidia majukumu mengi ya timu ni wakati wa makocha kujifunza kupitia makosa ya kumfanya acheze.

Aidha Tshishimbi amesema mbali na makocha pia viongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kuangalia jinsi ya makosa ya Morrison.

Advertisement

"Morrison hata nidhamu yake haikuwa sawa,unapokuwa unacheza mchezo mkubwa kama huu kuna heshima unayotakiwa kuonyesha.

"Viongozi wanatakiwa kujifunza jinsi ya kuishi na mchezaji husika,wanatakiwa kuangalia wamekosea wapi."

Advertisement