Tshabalala aeleza ya moyoni Simba

Muktasari:

Akizungumza na Mwanaspoti Tshabalala alisema; “Nafurahi kuwa hapa na pia kwangu mimi ni heshima kubwa kuchezea Simba, nitazidi kupambana kuhakikisha nakilinda kiwango changu ili nizidi kupata namba chini ya kocha yoyote atakayeinoa Simba.”

BEKI wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji ndani ya kikosi bora cha Simba.

Tshabalala miongoni mwa nyota wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja ana uhakika wa namba ndani ya kikosi chake licha ya kuwa na ushindani dhidi ya mkali mwenzie, Gadiel Michael, aliyetua kutoka kwa mahasimu, Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti Tshabalala alisema; “Nafurahi kuwa hapa na pia kwangu mimi ni heshima kubwa kuchezea Simba, nitazidi kupambana kuhakikisha nakilinda kiwango changu ili nizidi kupata namba chini ya kocha yoyote atakayeinoa Simba.”

Aidha Tshabalala anasema, katika kumbukumbu za maisha yake katika soka, hatasahau kuwa alikuwa sehemu ya wachezaji walioipeleka Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hili jambo halitafutika maishani mwangu, ni historia na itakuwa kumbukumbu yangu maishani,” alisema.

Nyota huyo amesisitiza mafanikio ambayo klabu yake inayapata yanatokana na umoja uliopo ndani ya timu yao kuanzia viongozi, wachezaji mpaka mashabiki wao.