Try Again yupo sana Simba

Muktasari:

Nyota wa zamani wa Simba na aliyewahi kuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Idd Pazi ‘Father’ aliliambia Mwanaspoti hakuna asiyefahamu umuhimu wa Try Again ndani ya klabu hiyo hata klabu hajakaimu madaraka hayo yaliyokuwa chini ya Evans Aveva.

KAIMU Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ aligoma kuchukua fomu ya kuwania nafasi kwenye Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Novemba 4, licha ya wadau mbalimbali kufanya juhudi za kumshawishi agombee.

Hata hiyo, imeelezwa licha ya kutojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, lakini Try Again ataendelea kuwemo ndani ya Simba akiwa na nguvu kubwa kutoka upande wa pili wa mwekezaji baada ya kugundua umuhimu wake katika kupambania maendeleo ya klabu.

“Try Again hata kama hataki na alikataa kuchukua fomu ila naamini atakuwa sehemu nyingine uongozi upande wa Mwekezaji, ni kiongozi mzuri, anaweza kusimamia jambo lake, wanachama wa Simba wasifikirie kumkosa mtu muhimu kama huyo, bali atakuwa upande wa pili ambao ni bora zaidi.

“Akiteuliwa upande wa Mwekezaji atafanya kazi vizuri zaidi ya kuisaidia Simba kupata maendeleo na mafanikio, hawezi kuwaangusha Wanasimba kwani yeye ni Simba wa muda mrefu na ana mapenzi nayo,” alisema Pazi

MKWABI,

MTEMI SAFI

Kuhusu wagombea nafasi ya Mwenyekiti, Pazi alisema “Nimefurahia sana uchaguzi wa sasa hivi kwani wagombea nafasi za juu ni wale ambao wanaufahamu mpira, wanajua maumivu ya wachezaji hivyo ni wagombea sahihi na yeyote kati ya hao atakayechaguliwa atafaa kuiongoza Simba.

“Ni watu wa kawaida sana ila wana akili nyingi ya soka, mambo ya pesa watasaidiana na wawekezaji ndio maana ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, kutakuwa na watafuta pesa na wanaofahamu soka vizuri, hivyo kila kitu kitaenda sawa.

“Upande wa wajumbe pia nimewaona kuna wazoefu wenye sifa za kuongoza Simba hata wanawake pia wamejitokeza ambao wana mapenzi na klabu na wanaufahamu mpira,” alisema Pazi Hilal ya Sudan Sudan na baadhi ya klabu huko Arabuni.