Tottenham kuvunja rekodi yake ya uhamisho

Thursday June 27 2019

 

TOTTENHAM baada ya kutosajili mchezaji yeyote katika madirisha mawili yaliyopita hatimaye inakaribia kuvunja rekodi yake ya uhamisho kwa kumchukua kiungo mahiri wa Lyon na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Tanguy Ndombele kwa dua linalokadiriwa kuwa ni Pauni 60 milioni.

Dau hilo litalipiku dau la Pauni 42 milioni ambalo Tottenham ililipa kwa Ajax kumchukua beki wa kimataifa wa Colombia, Davinson Sanchez miaka miwili iliyopita na hii inaashiria Spurs haitanii msimu huu.

Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas amekiri Ndombele anatakiwa na klabu nyingikubwa. Na mchezaji huyo anaonekana kutaka kutimka zake Lyon na klabu hiyo haiwezi kumzuia zaidi ya kumwachia mlango wazi.

Kuwasili kwa Ndombele kunaashiria ndio mwisho wa kiungo wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama ambaye alicheza kwa kusuasua msimu uliopita baada ya kupata majeraha na kuibuka kwa Harry Winks na huenda Wanyama naye akatimka klabuni hapo.

Advertisement