Torres ampa Klopp ubingwa England

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2007 akitokea Atletico Madrid na aliondoka siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo Januari 2011 kwenda Stamford Bridge kwa ada ya Pauni 50 milioni.

Tokyo, Japan, Mshambuliaji nguli wa Hispania, Fernando Torres, amesema anatamani kuona Liverpool ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu kuliko Chelsea.

Torres (34), ambaye Julai alijiunga na Sagan Tosu ya Ligi Kuu Japan, amefichua kuwa licha ya kupata mafanikio makubwa akiwa Chelsea, lakini hatasahau wema aliofanyiwa na mashabiki wa Liverpool.

“Nasema ukweli kutoka moyoni kuwa Liverpool na Chelsea zote nazipenda hata sijui ninaipenda ipi zaidi, lakini kwa sasa ninaiombea Liverpool ichukuwe ubingwa wa England kwasababu imekosa muda mrefu,” aliiambia Sky Sports.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2007 akitokea Atletico Madrid na aliondoka siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo Januari 2011 kwenda Stamford Bridge kwa ada ya Pauni 50 milioni.

Alisema Chelsea, ilimpa heshima ya aina yake katika maisha ya soka kwa kuwa alitwaa ubingwa wa la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa Ligi na Kombe la FA.

Torres alikosa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya msimu wa 2014-15 Chelsea ilipotwaa alipojiunga na AC Milan kwa mkopo.

“Ninatamani Liverpool itwae ubingwa wa England msimu huu kuliko Chelsea, imekosa muda mrefu licha ya kucheza vizuri chini ya Kocha Jurgen Klopp,”.

Torres, alitamba katika kikosi cha Liverpool akifunga mabao