Timu kibao zinamtaka Ozil, tatizo…

Muktasari:

 

  • Mwakilishi wa Ozil, Dr Erkut Sogut alisema kuwa mtu wake, moyo wake wote ameubwaga Arsenal, licha ya kupata ofa kibao kutoka nje ya Emirates.

London, England .UKISIKIA kubwagamoyo ndiko huku, wakala wa kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil amesema ana ofa ya Chinese Super League itakayomwacha njiapanda kabla ya kusaini Arsenal.

Mapema Januari, Mjerumani huyo alikuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi Gunners’ akivuna Pauni £350,000 kwa wiki.

Lakini mwakilishi wa Ozil, Dr Erkut Sogut alisema kuwa mtu wake, moyo wake wote ameubwaga Arsenal, licha ya kupata ofa kibao kutoka nje ya Emirates.

‘Ukweli kuna ofa kibao Asia, Ni ofa za maana. Lakini kwa Mesut, pesa kwake si suala la kipaumbele, anachotaka yeye ni kucheza,’ Sogut aliliambia Evening Standard.

‘Pesa ni eneo moja muhimu la kuangalia, lakini watu wanatakiwa kuangalia, suala la soka ni kwa watu kujinasibu kwa kuangalia wapi unacheza.

"Soka la biashara ni muhimu kwa sasa. Kuna mambo ya kuangalia," alisema.

‘Mesut ni mchezaji mwenye wafuasi wengi klabuni, hata ukiangalia mauzo ya jezi yake, ni babu kubwa.

‘Mwisho wa siku, Haya yote tunakaa tunyaangalia na kuyafanyia kazi.

‘Kwa hiyo suala la soka biashara ni kitu muhimu kwa Mesut, amecheza timu nyingi na ameonyesha kiwango kiasi cha kuaminiwa na kupewa jezi namba 10 Ujerumani.

‘Soko lake ni dunia nzima. Klabu inpata pesa kutokana na viyu vyake mbalimbali, lakini

‘Mesut ana uwezo wa kusaini klabu yoyote ile na akafanya vizuri, lakini tatizo ana mahaba na Arsenal. Ninemwambia kila jambo, lakini mwenyewe anaonekana anataka kubakia Arsenal.’