Thomas Partey ni Pauni 110 milioni

Wednesday October 07 2020
partey pic

LONDON, ENGLAND. USAJILI wa kiungo Thomas Partey umeripotiwa kuigharimu Arsenal mkwanja mrefu, Pauni 110 milioni ambayo italipa ndani ya miaka minne. Arsenal ilitangaza juzi Jumatatu imekamilisha usajili wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana baada ya kulipa Pauni 45 milioni zilizohitajika kuvunja mkataba wake huko Atletico Madrid.

Hata hivyo, ripoti zinadai dili hilo litaigharimu Arsenal Pauni 110 milioni kwa muda wake wa mkataba atakaokuwa Emirates. Arsenal kwanza imelipa Pauni 2.5 milioni ada ya usajili, pia itamlipa staa huyo mshahara wa Pauni 260,000 kwa wiki jambo linalofanya saini yake kwa miaka minne kuwagharimu Pauni 110 milioni.

               

Advertisement