Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dante aaga KMC akicha maswali aendako

DANTE Pict

Muktasari:

  • Dante alitoa shukrani za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na mashabiki wa KMC kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwa muda wote aliokuwepo klabuni hapo.

BEKI wa kati wa zamani wa Yanga, Vincent Andrew ‘Dante’ ametangaza kuachana na KMC yenye maskani yake Kinondoni baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka mitano.

Dante alitoa shukrani za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na mashabiki wa KMC kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwa muda wote aliokuwepo klabuni hapo.

“Ulikuwa wakati mzuri ndani ya kikosi cha KMC, miaka mitano nanyi sio midogo kwa maana nyakati zote tulizopitia. Sijutii kuwa sehemu ya kikosi cha Wana Kinondoni kwa muda wote nikitoa huduma yangu hapo. Ni wakati sasa wa kupata changamoto mpya mahali pengine,” alisema.

Dante ambaye aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kabla ya kujiunga na KMC mwaka 2020, ameweka historia ya kuwa mmoja wa wachezaji waliodumu kwa muda mrefu ndani ya kikosi hicho kinachomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Wakati akiwa KMC, beki huyo alijijengea heshima kwa kuwa kiongozi wa ulinzi akiongoza safu ya mabeki kwa utulivu na ukomavu mkubwa, hasa katika mechi ngumu dhidi ya vigogo wa soka nchini, Simba, Yanga na Azam.

Hata hivyo, hivi karibuni hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutoka na kusumbuliwa na majeraha ya hapa na pale Dante alikuwa msaada mkubwa kwa wachezaji chipukizi kwenye kikosi hicho kutokana na uzoefu alionao.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya mchakato wa kuijenga upya timu kwa msimu ujao.

Hadi sasa haijajulikana wazi Dante atajiunga na timu gani, lakini taarifa zimeanza kusambaa kwamba baadhi ya klabu kutoka Ligi Kuu na Championship zimeonyesha nia ya kumsajili, hasa kutokana na uzoefu wake wa ligi ya ndani na utulivu wake uwanjani.