Tenisi kutupa karata ya kwanza Afrika leo

Muktasari:

  • Mollel ambaye ameambatana na wachezaji, Kanuti Alangwa na Ester Nankulange anakwambia hawajaenda Tunisia kushangaa maghorofa.

TIMU ya Taifa ya Tenisi leo Jumatatu itaanza harakati za kusaka ubingwa wa Afrika kule Tunisi ambako kocha wa timu hiyo, Goodluck Mollel anakwambia hawafungwi kizembe.

Timu hiyo iliyoondoka nchini juzi Jumamosi itashiriki ufunguzi wa mashindano hayo leo na kwa mujibu wa kocha huyo watachuana katika staili ya mchezaji mmoja mmoja (singels).

Mollel ambaye ameambatana na wachezaji, Kanuti Alangwa na Ester Nankulange anakwambia hawajaenda Tunisia kushangaa maghorofa.

“Hatuwezi kutolewa kizembe, vijana wangu walipambana na kufuzu kushiriki mashindano haya, hivyo morali ile ile ndiyo tunakwenda nayo Tunisia,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA), Denis Makoye alisema matokeo mazuri watakayopata wachezaji hao yataiweka Tanzania katika viwango vya Tenisi Afrika.