VIDEO: Tarimba aifagilia Simba

Muktasari:

Simba walicheza fainali za kombe hilo dhidi ya Namungo ambapo walishinda bao 2-1, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

MKURUGENZI wa Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa, Abbas Tarimba amekiri kwamba hajawahi kusema Simba hoyee ila leo Jumatatu amekamatika.

Tarimba amesema hayo wakati wa mapokezi ya Simba waliotwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kuwa walichofanya Simba wanastahili pongezi kubwa, hivyo hajutii kutamka 'Simba hoyee.'

Simba walicheza fainali za kombe hilo dhidi ya Namungo ambapo walishinda bao 2-1, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

"Simba imetufanya wadhamini wao tujivunie kufanya kazi nao, si rahisi kuchukua mataji yote kwa msimu mmoja, wanastahili pongezi kubwa sana,"

Ameongeza kuwa "Katika maisha yangu ya soka sijawahi kusema Simba hoyee hii ni mara ya kwanza, hii inatokana na uwezo mkubwa ambao wamefanya,"

Amesema kwa jinsi ambavyo wamefanya vyema msimu huu, wanaamini wataendelea kufanya kazi nzuri ili kuhakikisha wanalifanya soka la Tanzania kusonga mbele.

Ukiachana na hilo, Tarimba amesema amefurahishwa na moyo wa upendo ambao ameuonyesha staa wa Simba, Mzambia Clatous Chama ambaye pesa aliyopewa ya mchezaji bora ameipeleka kwa watoto yatima.

"Amefanya kitu cha kuigwa, kwani watoto yatima wanastahili kufurahi na sisi pia kuwapa moyo wa kijituma kwamba kila kitu kinawezekana," amesema.

Ndani ya msimu mmoja, Simba wamekusanya mataji matatu ambayo ni Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Ngao ya Hisani na Kombe la ASFC