Taifa Stars mzuka umepanda yaikamia Kenya, Nyoni ndani

Thursday June 27 2019

 

By Khatimu Naheka

Cairo, Misri.Taifa Stars ndiyo Taifa Stars leo wanadakika 90 ngumu za kuamua kulinda heshima au kujihakikishia nafasi ya kurejea nyumbani watakapokutana na majirani zao Kenya 'Harambee Stars' katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Fianali za Mataifa Afrika.

Mchezo huu mezikutanisha timu jirani kisha kupewa jina la mechi ya watani wa jadi ambapo timu zote mbili zinahitaji matokeo ya ushindi kuweza kufufua matumaini ya kusonga mbele,baada ya zote kupoteza mechi za kwanza na  wakibakiza mechi moja mkononi.

Stars chini ya kocha Emanuel Amunike imekuwa katika maandalizi tofauti tangu ilipopoteza 2-0 dhidi ya Senegal,lengo likiwa ni kuirudishia ubora timu hiyo kabla ya kukutana na Kenya ha[po kesho katika Uwanja wa June 30.

Baada ya matokeo hayo mabaya Stars imekuwa ikipewa ushauri wa kisaikolojia kuhakikisha matokeo hayo yanaondoka katika akili za wachezaji ili kuweza kuppata ushindi.

Mbali na hilo pia makocha wa Stars wamekuwa wakiwaibgiza katika barafu wachezaji wote kila baada ya kipindi cha mazoezi yanapomalizika ikiwa ni mbinu za kupoza miili ya wachezaji kuondoa uchovu.

Hatua hiyo imewafanya wachezaji kuwa wachangamfu katika mazoezi ya siku mbili yanayofanyika katika Uwanja wa timu ya Petrojet klabu anayochezea kiungo Himid Mao.

Advertisement

Nyoni ndani

Mabadiliko makubwa katika kikosi cha kocha Amunike huenda tukakuona kiungo mkongwe Erastro Nyoni azkirejea uwanjani baada ya kukaa nje na kukosa mchezo wa kwanza kutokana na majeruhi.

Kurejea kwa Nyoni ambaye ana uwezo mkubwa wa kutuliza timu kumekuwa na furaha kwa makocha ambapo nafasi kubwa ni kwamba safu ya kiungo ya timu hiyo inaweza kuwa na mabadiliko.

katika mazoezi ya juzi usiku Amunike alitumia dakika 30 kuwapa mazoezi maalum viungo na safu ya ulinzi kuhakikisha wanakuwa na mabadiliko makubwa kabla ya mchezo huo wa kesho.

Amunike alionekana akiwa mkali zaidi kwa viungo wa kati Mudathir Yahaya,Himid Mao,Feisal Salum na Nyoni kuhakikisha wanakuwa na ubora anaoutaka katika kutekeleza majukumu yao huku akiwabadilisha mara kwa mara.

Huyu hapa Amunike

Akizungumzia mchezo huo Amunike alisema mechi hiyo ni wazi itakuwa ngumu lakini kila timu itakuwa na mbinu zake katika kutafuta ushindi.

Amunike alisema ameiona Kenya lakini ugumu wa timu hizo ni jinsi zilivyo karibu huku wachezaji nao wakijuana na kwamba wataingia katika mchezo huo na kiu ya kupata ushindi kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Alisema Kenya ni timu nzuri na hatua ya kupoteza mechi yao ya kwanza haina tiofauti na wao kufuatia kukutana na timu zenye uzoefu mkubwa lakini mechi baina yao iytakuwa na presha tofauti.

"Tumekuwa katika maandalizi mazuri baada ya mechi ya kwanza,tunapokutana na Kenya inakuwa ni mechi tofauti kutokana na ukaribu wa nchi hizi mbili,"alisema Amunike.

"Tunahitaji ushindi tyunatambua nao wanahitaji pia lakini kwetu tuna malengo yetu amnbayo ili tuyafikie tunahitaji matokeo mazuri,Kenya ni timu nzuri nafikiri itakuwa mechi ngumu,nawaamini wachezaji wangu."

Kenya nao wana malengo kama Stars na baada ya kupoteza mbele ya Algeria kiu yao ni kutafuta ushindi katika mchezo wa kesho utakaoanza majira ya saa mbili usiku hapa Cairo wakati Tanzania ikiwa saa nne usiku.

Wakiwa mazoezini kocha wa Kenya Mfaransa Sebastian Migne amekuwa akisisitiza kutaka kuona soka la kucheza pasi nyingi zinazokwenda mbele.

Mbali na hilo Mfaransa huyo amekuwa na muda wa kuwapa mbinu washambuliaji wake Michael Olunga na Francis Kahata kuhakikisha wanarejea katika ubora wa kufunga.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Migne alisema anatambua ugumu wa  mchezo huo na kwamba jambo zuri pekee liotakalowapa ushindi ni ubora wao wa kumiliki mpira.

Migne alisema ingawa ana changamoto ya maumivu madogo yua wachezaji wake lakini anaamini hilo litakuwa sawa kabla ya mchezo ujao huku akisema hawataidharau Tanzania katika mchezo huo.

"Tumatambua ugumu wa mchezo huo lakini tunahitaji kuwa na mabadiliko hasa juu ya kumiliki mpira,hii itatupa njia yas kupata matokeo tunayotaka,"alisema Migne.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisement