Sven kutokea hapa….

Friday October 23 2020
sven pic

ACHANA na matokeo iliyoyapata Simba katika mechi ya jana ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prison, kocha Sven Vandenbroeck ameweka wazi kuwa anataka kuona timu yake inacheza soka la kuvutia.

Soka la kuvutia na kumiliki mpira ambalo Sven amekuwa akitaka kuliona likichezwa katika kikosi chake ni kama lile ambalo wamekuwa wakilitandaza Barcelona kutokea Hispania.

Sven ameliambia Mwanaspoti ukifuatilia katika kila mechi iwe ya mashindano au kirafiki wamekuwa wakipiga pasi nyingi kuliko wapinzani wao jambo ambalo limekuwa likimvutia ingawa bado wachezaji wake hawajafika pale anapotamani kuona wanafikia.

“Unajua falsafa yangu ni kuona soka la kuvutia ambalo ndani yake tunatakiwa kumiliki mpira kuliko wapinzani wetu, kupiga pasi nyingi ambazo zitatupa njia ya kutengeneza nafasi za mabao na katika kumiliki mpira huku tutakuwa tunawapa wakati mgumu wapinzani ambao watakuwa wanapanga mbinu za kutuzuia kwanza.”

“Wachezaji wangu wameingia katika falsafa hiyo na ukiangalia pasi ambazo tumecheza katika mechi iliyopita ni ndogo kuliko mchezo ambao umefuata inakuwa zaidi ya zile na hilo ndio natakiwa kuliona tunafanya mara kwa mara tukiwa nyumbani au ugenini.”

“Tukicheza katika falsafa hii ya kumiliki mpira na kupiga pasi nyingi hata wapinzani muda mwingi watakuwa wanafikiria namna gani ya kutuzuia kuliko ambavyo tutakuwa tunawafikiria wao na hili tumekuwa tukilifanyia kazi mara kwa mara katika mazoezi yetu.”

Advertisement

“Ili kufanikiwa katika hili la kumiliki mpira na kucheza soka la kuvutia lazima ufiti wa kila mchezaji uwe tayari kwani muda wote tunatamani kuwa na mpira ikitokea kama kuna ambaye hayupo tayari tutashindwa kulitimiza hilo ndio maana muda mwingine tunacheza mechi za kirafiki na timu kama Mlandege ambayo wachezaji wake walitupa kipimo tosha katika kushindana.

“Tukifanikiwa katika kumiliki mpira muda mwingi kama ambavyo nahitaji katika falsafa yangu hata kukaba kutakuwa kuna pungua kwetu kwani muda wote mpira tutakuwa tunao na hiyo ndio itakuwa aina yetu ya kuwazuia wapinzani.”

Rekodi zinaonyesha katika mechi tano za ligi ambazo Simba imecheza zote imeongoza umiliki wa mpira mara baada ya dakika 90, kumalizika ikiwemo ya Ihefu ilimiliki kwa asilimia 57, Gwambina asilimia 63 na Biashara United ilimiliki kwa asilimia 64.