Hersi: Ugumu wa msimu umetufanya tufurahie

Muktasari:
- Hersi aliyasema hayo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1, jijini Dar es Salaam wakitokea Zanzibar ambako Yanga ilishinda 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mechi yao ya fainali ya Kombe la Shirikisho kupitia mabao ya kiungo Mkenya Duke Abuya na mshambuliaji Clement Mzize.
RAIS wa Yanga, Mhandisi Hersi Said amesema ugumu waliopitia msimu huu umewafanya leo kufurahia matunda.
Hersi aliyasema hayo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1, jijini Dar es Salaam wakitokea Zanzibar ambako Yanga ilishinda 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mechi yao ya fainali ya Kombe la Shirikisho kupitia mabao ya kiungo Mkenya Duke Abuya na mshambuliaji Clement Mzize.
Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za wachezaji na uongozi kwa ujumla, anawapongeza waandishi wa habari kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhabarisha watu.
"Ulikuwa msimu mgumu, tumepitia mambo mengi magumu, lakini tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kuibuka mabingwa," alisema Hersi na kuongeza: "Niwapongeze pia nyie waandishi wa habari mmekuwa kiungo muhimu wa ku
Yanga inafanya Parade kubwa kwa ajili ya kushangilia mataji yake matano ambayo imetwaa katika msimu huu wa 2024-25 ikiwa ni utamaduni ambao imeufanya katika misimu yote hii minne mfululizo ambayo timu hiyo ya wananchi imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.