Paredi la Yanga lawabeba bodaboda

Muktasari:
- Mwanaspoti lipo katika msafara huo, limeshuhudia baadhi ya mashabiki wakikubaliana bei na bodaboda ambao wanabeba abiria wqwiki hadi watatu kufukuzana na gari iliyobeba mataji sambamba na wachezaji.
KATIKA msafara wa Yanga, bodaboda wamepata fursa ya kubeba mashabiki kwa kujipatia kipato, kutoka kwa mashabiki ambao wamechoka kutembea na kuamua kutumia usafiri huo.
Mwanaspoti lipo katika msafara huo, limeshuhudia baadhi ya mashabiki wakikubaliana bei na bodaboda ambao wanabeba abiria wqwiki hadi watatu kufukuzana na gari iliyobeba mataji sambamba na wachezaji.
Kutokana na msafara kuwa na magari mengi yanayotembea taratibu, kumekuwa na foleni, inayosababisha bei kuchangamka.
Pamoja na bei wanazotajiwa haionekani kuwasumbua mashabiki waliojawa na shangwe ya kusherehekea ubingwa wa msimu huu, ukiwa wa mara 31 tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.
Haijafahamika ni kiasi gani wanatoa kukodi usafiri huo ambao umetawaka kwenye msafara wa sherehe za ubingwa wa Yanga.
Yanga inatembeza mataji matano iliyotwaa ndani ya msimu wa 2024-2025 likiwamo Kombe la Toyota ililotwaa Afrika Kusini, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ililotwaa usiku wa jana Jumapili kwa kuifunga Singida Black Stars kwa mabao 2-0.
Katika fainali hiyo ikliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Dube Abuya na Clement Mzize na kuipa Yanga taji la nne mfululizo la michuano hiyo na la tisa kwa ujumla tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1967.