Straika Kagera Sugar nje msimu mzima

Friday January 24 2020

Straika Kagera Sugar nje msimu mzima-MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Evaligestus Mujwahuki-pasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,-

 

By Saddam Sadick,Mwanza

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Evaligestus Mujwahuki atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima akiuguza jeraha la goti.
Mujwahuzi aliumia goti hilo Oktoba mwaka jana wakati timu yake ikicheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC ambapo waliibuka na ushindi wa bao 2-1.
Straika huyo mwenye kasi uwanjani alicheza mechi sita ambapo aliisaidia Kagera Sugar kuvuna pointi 12 na kukaa nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Mujwahuki amesema baada ya kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ripoti ya daktari imeeleza akwamba anapaswa kukaa nje kwa miezi tisa akiuguza jeraha lake.
Alisema licha ya kwamba alikuwa na mipango yake msimu huu, lakini anaona wazi kukwama na sasa anasubiri kujipanga upya na msimu ujao.
“Ni pigo kubwa kwangu kwa sababu mpira ndio kazi yangu, nilikuwa na ndoto nyingi ila ndio hivyo yametokea kwahiyo ni kujipanga tena na msimu ujao” alisema Mujwahuki.
Nyota huyo ambaye alisajiliwa na timu hiyo msimu huu akitokea Mbao FC, aliongeza kuwa anaamini atarudi kwenye ubora wake na kwamba atafanya kile alichoelekezwa na wataalamu.
“Kikubwa ni uvumilivu lakini kufanya kile nilichoelekezwa na wataalamu, ninaamini nitapona na kuendelea na majukumu yangu siwezi kukata tamaa,” alisema

Advertisement