Steve Nyerere afunguka kuhusu kuhamia Simba

Tuesday January 21 2020

Steve Nyerere afunguka kuhusu kuhamia Simba -Mchekeshaji Tanzania- Steve Nyerere-mitandao ya kijamii -

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Mchekeshaji Tanzania, Steve Nyerere amezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kupost video akisema amehamia kushabikia Simba akiachana na Yanga.

Katika video yake iliyosambaa kwenye mtandao wa kijamii Instagram ikisema "Mimi Steve Nyerere kwa akili yangu timamu, kuanzia leo na hamia Simba sports club asanteni"

Akizungumzia suala hilo Steve Nyerere amesema amefurahishwa na kitendo cha kueditiwa kwani amejiona angekuwa mchezaji angeuzwa bei ghali sana mchezaji wa kimataifa na kikubwa zaidi maisha ni Michezo maisha ni furaha japo hataweza kuhamia Simba kwani  yeye Yanga damu hawezi iacha yanga .

"Nashukuru mtu aliye edit video ya kusema mimi nahamia Simba sports club, ni kitu kibaya ni jambo la kumpongeza kwa kukaa kuchukua muda wake ameedit ameposti kitu kibaya.

“Maisha ni furaha na tunaposema Simba na Yanga wote tunategemeana kwahiyo nimefurahi hizi 'Joke ' sijachukulia 'siriaz' mimi ni Yanga damu, mimi ni mwananchi mimi ni timu ya wananchi na kamwe siwezi iacha yanga, yanga ni mimi na mimi ni yanga naipenda sana timu yangu

"Niseme tu unaweza kuzaa watoto watano au kumi usitegemee kupata watoto wote wawe kwenye mfumo wa akili moja, kwahiyo lazima upokee wote, sasa sisi  yanga tunapita kipindi kidogo cha majaribio ya kupokea, kwahiyo daima yanga mbele  nyuma mwiko ndio maana nasema nimependa zile 'Joke' na ndio zinatufanya tuishi na kuendelea kuwepo kwahiyo kwangu mimi ni faraja Kwa zile 'Joke'"amesema Steve Nyerere.

Advertisement

Video hiyo ilizua mjadala kwa mashabiki wa timu ya Simba na Yanga, ambapo mashabiki wa Simba wakidai kumpokea kwa mikono miwili msanii huyo huku wakisema ameisaliti timu yake ya Yanga.

 

Advertisement