Solskjaer amtolea macho beki Palace

Wednesday June 12 2019

 

London, England.Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameongeza kasi ya kupata saini ya beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka wa Crystal Palace.

Licha ya beki huyo wa kulia kuwekwa sokoni kwa Pauni50 milioni, kocha huyo amepania kumsajili katika majira ya kiangazi.

Palace imekataa ofa ya Pauni40 milioni iliyowekwa mezani na Man United.

Solskjaer ana kiu ya kufanya kazi na Wan-Bissaka baada ya kucheza kwa kiwango bora katika mashindano ya msimu uliopita.

Kocha huyo anataka beki wa kulia kuziba pengo la wachezaji wakongwe akiwemo nahodha Antonio Valencia na Ashley Young.

Kinda huyo wa timu ya Taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, amekuwa na msimu mzuri Palace.

Advertisement

Man United  ina orodha ya wachezaji inayowataka katika usajili wa majira ya kiangazi akina Thomas Meunier wa Paris Saint-Germain, lakini Wan-Bissaka ndio chaguo la kwanza.

Advertisement