Simba yaonyesha jeuri ya pesa

Muktasari:

Aidha msafara wa Simba umekuwa ukitanguliwa na gari aina ya Chevrolet ambayo nayo ni moja ya magari ya kisasa. Simba leo inateremka uwanjani kupepetana na Mbabane Swallows

Msafara wa Simba uliopo hapa Manzini hauishi maisha ya kubahatisha kwani wamekodi mabasi mawili yanayowapeleka na kuwarudisha kwenye hoteli ya kifahari waliyofikia mjini hapa.

Ingawa katika mji wa Manzini hakuna mabasi mawili ya kisasa mabosi wa Simba wakiongozwa na Mulamu Nghambi wamefanya ujanja wa mjini na kupata mabasi hayo aina ya Mercedes Benz.

Aina hiyo ya mabasi ndiyo yanayonekana ya watu wenye uwezo kwa hapa na inasemakana timu ambazo zimekuwa zikionekana kuyatumia ni zile za Arabuni zinazoweka kambi mjini hapa.

Aidha msafara wa Simba umekuwa ukitanguliwa na gari aina ya Chevrolet ambayo nayo ni moja ya magari ya kisasa. Simba leo inateremka uwanjani kupepetana na Mbabane Swallows