Simba, Yanga kumaliza ubishi Uhuru

Muktasari:

  • Baada ya miaka tisa kurudi  upya kwenye Uwanja wa Uhuru wenye historia kubwa ya mchezo huo wa watani wa jadi

Dar es Salaam. Baada ya miaka zaidi ya nane, Yanga na Simba zitacheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru, badala ya ule wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza uamuzi huo kutoka na uwanja wa Taifa kufanyiwa marekebisho hivyo hatutakuwa tayari kuchezewa mechi hiyo.

Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano na  waziri mwenye dhamana ya michezo, Dk. Harrison Mwakyemba, ameweka wazi juu ya mchezo huo kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

"Tayari waziri mwenye dhamana hiyo kwa kushirikiana na TFF, wamesema mchezo huo utakuwa Uwanja wa Uhuru, tofauti na minong'ono iliyokuwa inaendelea,"alisema .

Lucas alisema mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni  na viingilo vyake jukwaa kuu, itakuwa Sh 20000, na  mzunguko itakuwa ni Sh.10000.

Mara ya mwisho Simba na Yanga kucheza kwenye Uwanja wa Uhuru ilikuwa Aprili 27, 2008 matokeo ya mchezo huo timu hizo zilitoka suluhu.

Uwanja wa Uhuru ulifungwa kutumika kwa mechi za soka mwanzoni mwa mwaka 2011, kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya Beijing Construction kutoa China.

 Kutokana uamuzi huo klabu za Simba na Yanga zikalazimika kutafuta viwanja vingine nje ya Dar Es Salaam kwa ajili ya mechi zao za ligi huku mechi baina yao ikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamaji 23,000 na mabadiliko yaliyofanywa ni pamoja na sehemu za kukalia ambazo mwanzoni hazikuwepo , vyumba vya kubadilishia nguo za wachezaji.