Shindano la Shinda Mchongo wa Mwanaspoti ni moto!

Thursday July 11 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Kama ulikuwa ulikuwa hujui sasa hutakiwi kuchelewa kabisa kwani shindano la Shinda Mchongo wa Mwanaspoti linakwenda kubadilisha maisha yako.

Wengi walikuwa hawajui lakini baada ya kupata ukweli wa shindano hilo wanalichangamkia haswa kama ilivyo kwa mteja wa kila siku wa Mwanaspoti, Masoud Mbwana aliyekutwa Mnazi Mmoja akinunua gazeti la Mwanaspoti.

Masoud pamoja na kununua gazeti hili kila siku, kazi yake ilikuwa ni kusoma na kuweka stoo, lakini baada ya kuelimishwa namna ya ushiriki na kusoma kwake gazeti la Mwanaspoti linaweza kubadilisha maisha yake, akaamua kuongeza idadi ya manunuzi.

"Yaani ukija kwangu nimeyarundika tu. Hii kupuni nilikuwa naiona, lakini sikuwa najua naitumiaje, hivi nilivyojua naenda kuyachana yote na kuleta kupuni kwa wahusika, pia naweza kuongeza idadi ya manunuzi kwa ajili ya ushiriki zaidi,"alisema Mbwana.

Venda wa kuuza magazeti maeneo ya Posta Mpya anayejulikana kwa jina la Juma, baada ya kugundua siri ya shindano la Shinda Mchongo wa Mwanaspoti aliamua kuwa mteja ghafla. Alinunua gazeti na kuchana kupuni ya shindano hilo akawapa wagusika.

Sehemu ya zawadi ambazo zinapatikana katika shindano hilo ni pesa taslimu na pikipiki kila wiki, wakati washindi wa wiwili wa droo ya mwisho watagawana kiasi cha shilingi milioni 10.

Advertisement

Namna ya kushiriki ni kununua gazeti ambalo linakuwa na tiketi kwenye ukurasa wa pili. Utaichana na kumpa aliyekuuzia gazeti au utaipeleka kwenye Ofisi za Mwanananchi Communications LTD.

 

 

 

 

 

 

Advertisement