Shabiki wa Simba atajirika na M-Bet

Muktasari:

Muray amesema kuwa mbali ya kujiendeleza katika masuala ya kilimo, pia atafungua ofisi ili kufanya shughuli zake za kilimo na biashara kisasa zaidi.

Dar es Salaam. Shabiki wa Simba, Arsenal na Real Madrid, Simon Eusebi Muray (32) ameshinda kitita cha Sh 81,097, 540. Baada ya kutabiri kwa baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa Kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake leo Alhamisi Februari 21, Muray ambaye ni mkazi wa Katesh, Hanang, mkoa wa Manyara amesema kuwa atatumia fedha hizo kuongeza mashamba ya vitunguu, kuboresha nyumba yake na kupanua duka la bidhaa za rejareja kuwa la jumla.

Muray amesema kuwa mbali ya kujiendeleza katika masuala ya kilimo, pia atafungua ofisi ili kufanya shughuli zake za kilimo na biashara kisasa zaidi.

“Nina mashamba ya vitunguu eneo la Mkalama, mkoa wa Singida ambayo kutokana na mtaji huu, nitaongeza wigo wa kilimo na vile vile kuboresha nyumba yangu. Nataka kuwa mkulima wa kisasa na mwenye malengo ya kufanya vyema katika sekta hiyo huku nikifanya biashara zangu,” alisema Muray.

Alisema kuwa alipokea taarifa za ushindi kwa furaha sana kwani katika maisha yake, hakutarajia kupata kiasi hicho cha fedha.

“Pia nitamwamisha mtoto wangu wa kutoka shule ya kawaida na kwenda ya kimataifa. Huu ni ushindi wa maana sana kwangu kwani kwa kutumia  sh1,000 kushinda kiasi hiki kikubwa cha fedha, ni faraja kubwa sana kwangu, nilianza kucheza muda mrefu na nilibishana na afisa wa M-Bet kwani niliamini kuwa ni matapeli,” alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Murray anakuwa anakuwa mshindi wa pili wa mwaka huu ikiwa mshindi wa pili kushinda kiasi kikubwa cha fedha tokea kuanza mwaka huu.

 “M-Bet ni nyumba ya mabingwa na Murray amejiunga tena na nyumba ya mabingwa kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitabili maisha yake, tunawaomba Watanzania kucheza michezo ya M-Bet ili kuweza kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kuanza maisha mapya,” alisema Mushi.

Naye, Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala alimpongeza Muray kwa ushindi na pia kuipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri kwa serikali.