Serengeti Boys yajifua maandalizi Afcon

Muktasari:

Dk Mwakyembe alisema mwezi ujao timu hiyo itakwenda Uturuki ambako imealikwa kushiriki mashindano maalum yaliyoandaliwa kule.

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys  imeendelea na  mazoezi  kwenye kambi jijini Arusha leo Alhamisi Uwanja wa Agha Khan kujiandaa na fainali za Afrika kwa Vijana U17, zitakazofanyika Aprili na Tanzania ikiwa mwenyeji.

Fainali hizo zitafanyika kwa wiki mbii kuanzia Aprili 14 huku zikishirikisha nchi nane ambazo ni Tanzania, Nigeria, Uganda, Angola, Senegal, Morocco, Cameroon na Guinea.

Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema serikali imejipanga kuhakikisha Serengeti Boys inafanya vyema katika mashindano hayo.

Dk Mwakyembe alisema mwezi ujao timu hiyo itakwenda Uturuki ambako imealikwa kushiriki mashindano maalum yaliyoandaliwa kule.

Alisema kuwa halitakuwa jambo la kupendeza kwa Serengeti Boys kufanya vibaya katika mashindano.

Kwa sasa timu hiyo ipo kambini kwa wiki nne.