Samatta atimiza ndoto, aitungua Liverpool

Wednesday November 6 2019

Kocha wa Liverpool -Jurgen Klopp-wachezaji -KRC Genk-ushindi -Samatta- atimiza- ndoto-aitungua- Liverpoo- Ligi ya -Mabingwa -Ulayal

 

London, England. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema wachezaji wamefanya kazi nzuri baada ya kupata ushindi dhidi ya KRC Genk.

Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta alitimiza ndoto yake baada ya kufunga bao dakika ya 40. Katika mchezo wa kwanza Genk ilifungwa 4-1.

Samatta aliweka ahadi ya kuifunga Liverpool katika mchezo huo baada ya kupata uzoefu katika mechi ya awali ambayo alikabiliana na beki nyota Virgil Van Dijk.

Liverpool ikiwa nyumbai Uwanja wa Anfield ilishinda mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mabao ya Georginio Wijnaldum na Alex Oxlade-Chamberlain yaliiweka kileleni Liverpool katika Kundi E.

 “Kazi imefanyika ingawa kundi letu halitabiriki lakini jambo la msingi ni kupata ushindi, matokeo ni matokeo tu,”alisema Klopp.

Advertisement

Kocha wa Genk Felice Mazzu wachezaji wake walicheza kwa kiwango bora baada ya kupata taabu katika mechi zilizopita.

“Najivunia wachezaji wangu. Tumecheza kamari kucheza na moja ya timu bora duniani, hakika tumecheza vizuri,”alisema Mazzu.

Advertisement