Refa wa ‘kona bao’ apewa fainali FA

Muktasari:

Fainali hiyo ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itachezwa katika dimba la Nelson Mandera, Sumbawaga Agosti 2, 2020

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza majina ya waamuzi sita watakaochezesha mchezo wa fainali kombe la Azam (ASFC).

Mchezo huo, utakaofanyika Jumapili Agosti 2, 2020 kati ya Namungo na Simba Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Waamuzi waliopewa jukumu la kusimamia mchezo huo yupo, Abubakar Mturo kutoka Mtwara, Abdallah Mwinyimkuu (Singida), Ahamed Arajiga (Manyara), Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam), Abdulaziz Ally (Arusha), na Hamdan Said kutoka Mtwara.

Mtathimini wa waamuzi katika mchezo huo atakuwa, Soud Abdi ambaye ni mwenyekiti wa chama cha waamuzi, na Israel Mjuni atakuwa Mkufunzi wa viungo.

Mturo alifungiwa miezi mitatu kuanzia Februari baada ya kushindwa kumudu mchezo kati ya Yanga dhidi ya Lipuli.

Mturo, Mwinyimkuu na Kayoko walikuwa kuwenye mchezo wa nusu fainali wakati Simba ikiichapa Yanga 4-1 Uwanja wa Mkapa Julai 12.