Rasmi Msimu mpya EPL Septemba 12

Friday July 24 2020

 

HATIMAYE majibu ya swali lililokuwa linaulizwa na mashabiki wengi wa Ligi Kuu England sasa yamejibiwa baada ya chama cha soka nchini humo kukaa kikao na wamiliki wa klabu za Ligi Kuu, ambapo miongoni mwa maadhimio yake yalikuwa ni kuamua tarehe rasmi ya kuanza kwa michuano hiyo katika msimu ujao.

Katika taarifa ambayo imetolewa na chama hicho inasema kuwa kuwa msimu mpya wa 2020-2021, utaanza Septemba 12, mwaka huu. Pia inatarajiwa kumalizika Mei 23, 2021 lakini bado viongozi wa chama hicho wanashauriana ili kupanga tarehe mpya ya michuano ya FA na EFL.

Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika Jumapili ijayo huku bingwa akiwa ni Liverpool ambaye amechukua taji hilo baada ya zaidi ya miaka 30 kupita tokea msimu wa 1980-90.

Tarehe ya kuanza tena kwa ligi hiyo imetajwa mapema zaidi kulinganisha na ligi nyingine ambazo licha ya bingwa mpya kujulikana lakini bado ratiba inasuasua, utaratibu huo umekuwa ni wa muda mrefu kwa Ligi Kuu England.

Advertisement