Rais Barca ajiwahi kabla ya kura

Barcelona, Hispania. Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amewasilisha barua ya kujiuzulu kuiongoza klabu hiyo, klabu imethibitisha.

Bartomeu anaaminika kukabidhi barua hiyo Jumanne jioni kabla ya upigwaji wa kura za kutokuwa na imani naye kumuondoa.

Taarifa ya klabu hiyo katika mtandao wa Twitter ilisomeka: “Rais Josep Maria Bartomeu ametangaza kujiuzulu kwake katika bodi ya wakurugenzi ya Barcelona.”

Gazeti la Sport in Spain ilisema wakurugenzi wa ilikuwa katika mchakato wa kupiga kura yan kutokuwa na imani baada ya kuwa kwenye malngo wa kutoka Nou Camp tangu timu ilipofungwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Real Madrid.

Bosi huyo raia wa Hispania mwenye miaka 57, alikuwa katika hali mbaya tangu sakata la kuandika barua ya kuondoka la mshambuliaji wao, Lionel Messi.

Baada ya majadiliano ya klabu na wachezaji, Messi aliamua kuandika barua ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo.

Mazungumzo kati ya baba wa Messi na Bartomeu yalishindwa kuzima uamuzi wa mshindi huyo wa mataji sita ya Ballon d’Or ya kuikacha klabu hiyo aliyoichezea kwa miaka 20.

Lakini baadaye, Messi aliamua kubadili uamuzi wake na kuendelea kubaki Barca kwa kuitumikia mwaka mmoja uliobaki katika mkataba wake wa sasa.

Mashabiki walikusanyika katika uwanja wa klabu hiyo kupinga uamuzi wa Messi wa kuondoka na kumtaka Bartomeu kuondoka.