Pogba aingia kikosi bora cha mwaka cha PFA

Thursday April 25 2019

 

London, England. Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ametajwa katika kikosi cha mwaka cha PFA Team 2018-19 – akiwa ni mchezaji pekee aliyetoka nje ya Manchester City na Liverpool.

City ina wachezaji sita kati 11, baada ya kupigiwa kura na wachezaji wenzao- kipa Ederson, beki Aymeric Laporte, viungo Bernardo Silva na Fernandinho na washambuliaji Sergio Aguero na Raheem Sterling.

Wachezaji wanne waliobaki wote wanatoka Liverpool ambao ni mabeki Andrew Robertson, Trent-Alexander Arnold, na Virgil van Dijk pamoja na mshambuliaji Sadio Mane.

Mshindi wa msimu uliopita mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah pamoja na nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang wote wakiwa wamefunga mabao 19, msimu huu wameshindwa kupenya katika kikosi hicho.

Nyota wa Tottenham, Harry Kane mabao 17 na winga Chelsea, Eden Hazard akiwa wamefunga mabao 16, katika ligi lakini wameachwa nje.

Timu ya mwaka ya PFA inatokana na kura zinazopigwa na Shirikisho la Wachezaji wa Kulipwa linaloundwa na wachezaji wenyewe.

Advertisement

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Manchester City kutoa wachezaji wengi katika timu hiyo msimu wa 2017-18 ilitoa wachezaji watano kati 11.

Hata hivyo, ni Sergio Aguero pekee aliyefanikiwa kurudi katika kikosi hicho baada ya miezi 12.

Advertisement