Ondoa Lukaku na Matic, nunua N’Golo Kante

Muktasari:

  • Sharpe anaamini kwamba mastaa wawili wa United, Romelu Lukaku na Nemanja Matic hawana mchango mkubwa katika kikosi cha Manchester United na wanaweza kuondolewa kwa ajili ya kumpisha kocha, Ole Gunnar Solskjaer kukisuka upya kikosi cha United kwa ajili ya EPL.

STAA wa zamani wa Manchester United, Lee Sharpe anaamini klabu yake hiyo inapaswa kuachana na mastaa wake wawili, Romelu Lukaku na Nemanja Matic na kuelekeza nguvu zao kumchukua kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante.

Sharp anaamini kwamba kocha wa Chelsea, Mauricio Sarri hamkubali sana Kante ambaye amemuhamisha nafasi yake na kumpeleka mbele huku akimtumia Jorginho katika nafasi yake na anaamini kwamba Sarri anaweza kushawishika kumuuza Kante.

Sharpe anaamini kwamba mastaa wawili wa United, Romelu Lukaku na Nemanja Matic hawana mchango mkubwa katika kikosi cha Manchester United na wanaweza kuondolewa kwa ajili ya kumpisha kocha, Ole Gunnar Solskjaer kukisuka upya kikosi cha United kwa ajili ya EPL.