Okwi, Juuko kuibeba Uganda Afcon

Muktasari:

Uganda ‘The Cranes’ ipo Kundi A pamoja na wenyeji Misri, DR Congo, na Zimbabwe. Wataanza mashindano kwa kucheza dhidi ya DR Congo Juni 22

Cairo, Misri. Uganda imetangaza kikosi chake cha wachezaji 23 tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika.

The Cranes ipo Kundi A pamoja na wenyeji Misri, DR Congo, na Zimbabwe. Wataanza mashindano kwa kucheza dhidi ya DR Congo Juni 22, kabla ya kuivaa Zimbabwe na kumaliza na Misri kati ya Juni 26 na Juni 30.

Kocha huyo wa zamani wa Ismaily, Sebastien Desabre amemwita mshambuliaji mwenye miaka 23, Derrick Nsibambi katika kikosi chake.

Kikosi hicho kinaongozwa na kipa wa Mamelodi Sundowns, Denis Onyango, nyota mzaliwa wa Sweden, Brian Mukiibi, Yeovil Town, Bevis Mugabi, Faruku Miya, Joseph Ochaya, na Isaac Muleme ni miongoni wa nyota wanaocheza nje Uganda.

Kikosi:

Makipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns, South Africa), Jamal Salim (Al Hilal-Sudan), Robert Odongkara (Adama City, Ethiopia).

Mabeki: Nico Wakiro Wadada (Azam, Tanzania), Brian Ronald Ddungu Mukiibi (Ostersunds, Sweden), Murushid Jjuuko (Simba, Tanzania), Bevis Mugabi (Yeovil Town, England), Isaac Muleme (FK Viktoria Zizkov, Czech Republic), Hassan Wasswa Mawanda (hana timud), Joseph Ochaya (TP Mazembe, DR Congo), Timothy Denis Awanyi (KCCA FC, Uganda), Godfrey Walusimbi (hana timu).

Viungo:  Mike Azira (Montreal Impact, Canada), Allan Kateregga (Maritzburg, South Africa), William Kizito Luwagga (Shakhter Karagandy, Kazakhstan), Khalid Aucho (Church Hill Brothers, India), Faruku Miya (HNK Gorica, Croatia), Abdul Lumala (Syrianska, Sweden), Tadeo Lwanga (Vipers SC-Uganda).

Washambuliaji: Patrick Henry Kaddu (KCCA FC, Uganda), Derrick Nsibambi (Smouha, Misri), Allan Kyambadde (KCCA FC Uganda), Emmanuel Arnold Okwi (Simba, Tanzania).