Njohole wa Mbao ajiweka sokoni

Muktasari:

  • Njohole aliibuka mchezaji bora wa mashindano ya SportPesa Supar Cup na kukabidhiwa hundi ya dola 500, katika mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Dar es Salaam. Kiungo wa Mbao FC, Ibrahim Njohole amemaliza mkataba wake na timu hiyo na yupo tayari kutafuta changamoto katika klabu nyingine za Ligi kuu.

Njohole aliibuka mchezaji bora wa mashindano ya SportPesa Supar Cup na kukabidhiwa hundi ya dola 500 za kimarekani, katika mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Njohole alisema umoja ushirikiano ndio siri ya mafanikio yao kubakiza Ligi Kuu na anawashukuru viongozi pamoja na wachezajhi wenzakje kwa ushirikiano waliokuwa wanampa walivyokuwa pamoja.

"Mkataba wangu umemalizika na hadi sasa hakuna kiongozi yeyote aliyenipigia kwaajili ya mazungumzo hivyo nikiwa kama mchezaji na mpira ndio ajira yangu napenda kuweka wazi kuwa kama kuna timu itahitaji huduma yangu nipo tayari kwa mazungumzo."

"Hata waajili wangu wa zamani kama wanaona umuhimu wangu kikosini bado upo pia milango ipo wazi ya kukaa meza moja na mimi kwaajili ya mazungumzo yatari kwa msimu mpya wa ligi kuhusiana na ofa kutoka timu nyingine nadhani hawana taarifa kama nimemaliza mkataba kupitia nyinyi ndio wanaweza kunitafuta baada ya kuweka wazi kuwa nipo huru kwa mazungumzo na klabu nyingine yeyote," alisema Njohole.