Niyonzima aitia presha Yanga

Sunday July 5 2020

 

By THOBIAS SEBASTIAN

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima ameshindwa kuendelea katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, ambao unaendelea muda huu katika uwanja wa CCM Karume mkoa wa Mara.

Niyonzima aliumia dakika ya nne, katika harakati ya kuwania mpira na wachezaji wa Biashara United, akadondoka chini na Daktari wa Yanga, Sheikh Mngazija aliingia uwanjani kumpatia matibabu na huduma ya kwanza.

Baada ya matibabu hayo mafupi Niyonzima alitolewa nje ya Uwanja na dakika chache baadaye alirudi uwanjani lakini alionekana kushindwa kuendelea na mechi baada ya kudondoka chini na watu wa huduma ya kwanza walikwenda kumbeba na machela.

Dakika ya nane, Niyonzima alitolewa akiwa amebebwa katika machela na nafasi yake kuchukua kiungo, Mzanzibar Abdulaziz Makame 'Bui'.

Advertisement