Ngoma aanza, Chirwa nje Azam ikivaa Ndanda

Muktasari:

Kuanza kwa Ngoma kuna mtoa Obrey Chirwa katika kikosi cha kwanza ambapo alikuwa amezoeleka kuanza na Richard Djodi.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Donald Ngoma ameanza katika kikosi cha kwanza cha Azam kitakachoanza dhidi ya Ndanda FC leo saa 1:00 usiku mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania ukatakaochezwa kwenye Uwanja wa AzamComplex, Chamazi.

Kocha Etienne Ndayiragije katika safu ya ushambuliaji amewaanzisha washambuliaji Donald Ngoma na Richard Djodi.

Kuanza kwa Ngoma kuna mtoa Obrey Chirwa katika kikosi cha kwanza ambapo alikuwa amezoeleka kuanza na Djodi.

Pia katika nafasi ya goli kipa kamuaanzisha Mwadini Ally na kumuondoa kabisa katika kikosi Razak Abarola ambaye amekuwa akianza mechi za Ligi na zile za kombe la Shirikisho.

Kikosi kamili Mwadini Ally, Nicco Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Daniel Amoah, Mudathir Yahya, Salum Abubakari 'Sure Boy', Frank Domayo, Donald Ngoma, Richard Djodi na Idd Seleman 'Nado'.

Benchi ni Benedict Haule, David Mwantika, Idd Kipagwile, Obrey Chirwa, Shabani Chilunda, Emmanuel Mvuyekure na Joseph Mahundi.