Newcastle, West Ham zajitosa kumsaka Samatta

Muktasari:

Wakati wa dirisha la kiangazi Samatta alihusishwa na kutakiwa na klabu tatu za England, West Ham United, Everton na Burnley.

London, England. Newcastle na West Ham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta baada ya kufunga bao dhidi ya Liverpool.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, Jumanne alifunga bao dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa timu yake ikifungwa 2-1.

Gharama za kumnunu pamoja na mkataba wake kwa sasa nai pauni 10milioni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.

Samatta mfungaji bora wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu uliopita akifunga mabao 25 na kuiongoza Genk kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Mtanzania huyo tayari amefunga mabao sita katika michezo 13 ya ligi aliyocheza hadi sasa, huku akifunga mabao mawili katika Ligi ya Mabingwa.

Wakati wa dirisha la kiangazi Samatta alihusishwa na kutakiwa na klabu tatu za England, West Ham United, Everton na Burnley.

Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao.

Samatta, mwenye kimo cha futi 5 inchi 11, amefunga mabao sita katika ligi ndogo ya klabu barani Ulaya, Europa League, na ni hapo ameanza kuonekana na klabu za England.

Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga 'hat-trick' dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5-2.

Gazeti la Daily Mirror liliripoti kwamba West Ham wanamfuatilia mchezaji huyo ingawa walisema Everton wanaonekana kuwa nafasi kubwa ya kumsajili  Januari.

Everton tayari wana uhusiano na Afrika Mashariki kupitia mdhamini wao SportPesa, na waliibuka kuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kuchezea Afrika Mashariki walipocheza dhidi ya mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia katika Kombe la SportPesa Super Cup mwaka jana.