Ndo hivyo, Eden Hazard, Madrid washamalizana

Wednesday May 15 2019

 

LONDON,England.KUMEKUWA na tetesi nyingi juu ya nyota wa Chelsea, Eden Hazard kuhamia Real Madrid msimu unaokuja na mchezaji huyo sasa ametia mafuta katika utambi baada ya kusema kuwa ameshafanya maamuzi na anasubiri kuona nini kinaendelea uopande wa pili.

Alisema hataki kukaa akiwaza atacheza wapi msimu ujao, anataka suala lake limalizike mapema iwezekanavyo. Kuna wakati mazungumzo yalikuwa yakiendelea kati ya klabu yake na Real Madrid lakini yakasimama.

Hukusu hilo Hazard alianika; “Nataka mambo yaishe, nataka kujua nini kitaendelea baadaye. Nafahamu hata mashabiki wanataka kujua nini hatima yangu.

“Viongozi wa klabu yangu wanaafahamu uamuzi wangu. Nilishawajulisha tangu wiki mbili zilizopita. Nipo hapa nasubiri maamuzi ya mwisho. Nataka kujua nini kitaendelea katika soka langu katika msimu unaokuja.

“Hata hivyo, nataka kuwaambia huwa nafikiria zaidi soka langu kuliko kitu kingine. Ninapokuwa uwanjani huwa najitoleo kwa kadri ya uwezo wangu kufanya mambo yaende sawa. Huwa nasahau kila kitu kinachoendelea kuhusu mkataba.” Hata hivyo, habari kutoka Real zinasema mchezaji huyo amekubali dili la Pauni 86 milioni na klabu hiyo itamtangaza baada ya fainali ya Europa kati ya Chelsea na Arsenal.

Imefahamika mchezaji huyo alikubali dili hilo wiki moja iliyopita.

Advertisement