Mzee Yusuf awapigia Dua waliomvamia

Friday January 11 2019

 

By Rhobi Chacha

Aliyekuwa mwimbaji taarabu, Mzee Yusuf amesema anawapigia dua watu waliomvamia.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mzee Yusuf amesema hatawaacha hivihivi waliomvamia kwani atawasomea dua kwa muda wa masaa matatu.
Aidha amesema dua hiyo sio albadiri ambayo inasifika kuua, bali ni dua ya kawaida ambayo nao alivyoteseka yeye na familia yake siku walipovamiwa.
"Kiukweli sitaweza kuwaachia watu walionivamia na kuweza kunipa hasara na majeraha mimi na mke wangu,nasema wazi kabisa nahakikisha nitakaa chini kwa muda wa masaa matatu kuwasomea dua watu walionivamia. Dua hiyo ni ya saa tatu na sio albadili ya kuua hapana. Mimi sitawaua ila cha moto watakiona. Kama wamezoea kuwachezea watu wageni wakiingia kwenye mji wao basi kwangu na mimi ni mwenyeji mwenzao wajue hilo,"alisema Mzee Yusuf.
Aidha Mzee Yusu aliongezakusema kuwa, anatatufa  kundi  linalokomesha hawa watu waliozoea kuvamia watu,maana siku zote wanaojifanya wasela huwa wanawasela wenzao na hii nia yake kuwakomesha.
Mzee Yusuf alivamiwa Januari 7, 2019 usiku wa kuamkia Jumatatu nyumbani kwake Chanika Buyuni Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo wezi hao walivamia na kufanya umafia ikiwemo kumjeruhi mkewe Leila Rashid sehemu mbalimbali za mwili wake na kufanikiwa kuiba saa, pete moja, viatu na pesa.

Advertisement