Wanamichezo wahimizwa kunywa maziwa kwa afya

Muktasari:

Bonanza la maziwa ili kuhamasisha wanamichezo hapa nchini wanapofanya mazoezi na kazi za mikono waelewe virutubisho vinapungua vikiwemo maji, protein na wanga hivyo wanapokunywa maziwa ya kutosha virutubisho vyote vinarudi

Dar es Salaam.Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema kila Jumapili ya mwisho wa mwezi watakuwa wanafanya mazoezi kuanzia Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya maonyesho Sabasaba lengo la kuhamasisha wanamichezo wanatumia bidhaa mbalimbali ikiwemo maziwa.

Akizungumza hayo Lyaniva alipokuwa kwenye bonaza la maziwa linalohamasisha mwanamichezo anapomaliza kufanya mazoezi anatakiwa kunywa maziwa kwa ajili ya afya yake.

Lyaniva alisema kila jumapili ya mwisho wa mwezi watakuwa wanafanya mazoezi hayo ambapo wanamichezo watakuta bidhaa mbalimbali yakiwemo maziwa zinazotengenezwa na vijana wa jogging hivyo wanapomaliza kufanya mazoezi hayo watanunua.

‘Haya maonyesho ambayo yanatokana na viwanda vyetu vya ndani ya nchi kuonyesha wanatengeneza nini nimeona viwanda vya maziwa ambapo wanamichezo wetu watakapomalizia michezo yao hapa watakunywa maziwa,’alisema Lyaniva

Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sophia Mlote alisema wameanzisha bonanza la maziwa ili kuhamasisha wanamichezo hapa nchini wanapofanya mazoezi na kazi za mikono waelewe virutubisho vinapungua vikiwemo maji, protein na wanga hivyo wanapokunywa maziwa ya kutosha virutubisho vyote vinarudi.

“Kauli mbiu yetu ya mwaka huu ‘tucheze tufanye mazoezi, tunywe maziwa ya afya bora’, katika unywaji wa maziwa tumeona kila mtanzania kwa wastani kwa mwaka anakunywa lita 49 ni kinyume na ushauri wa Shirika la Afya Duniani na Shirika la Chakula Duniani hivyo kwa wastani mtu anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka,”alisema Dk Mlote.

Alisema Tanzania kuna ngo’mbe wa maziwa na zaidi ya 1.2 milioni pamoja na wa asili jumla wapo 32.2 milioni wanatoa maziwa lita 2.7 bilioni na kwenye usindikaji vipo viwanda 99 kati ya hivyo vikubwa ni vitanoambapo wanasindika lita 194,000 ambazo ni kidogo.

Mwenyekiti wa Jogging wilaya ya Temeke,Musa Mtulia alisema mchezo huo umekuwa wenye amasa hivyo wanahamasisha michezo na uchumi kwa kuwa wana viwanda kupitia mchezo wa Jogging.

Alisema wapo kwa ajili ya kuhamasisha tamasha la maziwa kwa kuwa mazoezi hayo siyo kutengeneza afya lakini kuonyesha umuhimu wa mazoezi wanayoyafanya na lishe wanayotakiwa wapate kama wanamichezo.

“Leo hii tumeona bodi ya maziwa ipo hapa makampuni mbalimbali yanayozalisha maziwa wamekuja kutuonyesha vitu muhimu wanavyotaka tuvitumie baada ya kumaliza mazoezi yetu,”alisema Mtulia.