Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco: Pengo la Okwi halijazibwa Simba SC

Muktasari:

Okwi aliondoka Simba mwishoni mwa msimu na kutimkia klabu ya Ittihad iliyopo jiji la Alexandria nchini Misri na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Dar es Salaam.Nahodha wa Simba, John Bocco amesema pengo la Emmanuel Okwi bado linaonekana ndani ya kikosi chao na ndio sababu ya wao kushindwa kufunga mabao mengi.

Msimu uliopita safu ya ushambuliaji ya Simba ilifunga jumla ya mabao 53 huku Bocco akifunga mabao 14, Okwi (16) na Meddie Kagere mabao 23.

Bocco jana aliifunga bao moja Simba ikishinda 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi na kufuzu kwa nusu fainali.

Nahodha huyo alisema Okwi bado anahitajika kwenye kikosi chao licha ya Kagere kufanya vizuri, lakini mapungufu yaliyopo kwenye safu ya ushambuliaji yanaonyesha pengo la Mganda huyo.

Bocco alisema Okwi alikuwa haziachi nafasi anazozipata, tofauti na Kagere ambaye akitengenezewa nafasi tano basi yeye atafunga mbili au moja.

“Siyo kama Kagere afanyi vizuri hapana, Kagere ni mshambuliaji mzuri, lakini tofauti na Okwi ambaye hajawahi kupoteza nafasi hata moja anayotengenezewa amekuwa hafanyi makosa sehemu za hatari tofauti na Kagere,” alisema Bocco.