Mandojo, Domokaya waeleza walivyozamia tamasha la Wasafi

Wednesday November 13 2019

Mwanaspoti-Mandojo-Domokaya-Tanzania-TID-waeleza-walivyozamia-tamasha-la-Wasafi

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Wanamuzikii Mandojo, Domokaya wamesema walivamia tamasha la wasafi bila waandaaji kujua lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Wanamuziki hao wameyasema hao leo Novemba 13, 2019 katika mahojiano maalum walipotembelea ofisi za Mwananchi wakiwa wameambatana na mwanamuziki T.I.D.

Mandojo na Domokaya wamesema kama siyo TID wasingeweza kuingia katika tamasha hilo lililofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya posta Jijini Dar es Salaam.

Mandojo amesema katika umoja wao wamekubaliana kusaidiana kila kunapotokea onyesho na mmoja wao kualikwa.

“Wamekubaliana mtu anapokuwa na shoo mahali basi siyo mbaya kusindikizwa na wenzake.

“Hivyo siku ile ya tamasha T.I.D aliamua kumega muda aliopewa kupanda jukwaani na kutupa sisi na tunashukuru shangwe zilikuwa za maana jambo linaloonyesha watu bado wanatuhitaji sema sehemu ya sisi kuonekana na hakuna,”amesema Mandojo.

Advertisement

Naye Domokaya amesema waandaaji wa matamasha wanatakiwa wasiwasahau wasanii kama wao kwa kuwa bado wanamashabiki wao.

Hata hivyo wamesema wanashukuru baada ya tamasha hilo, uongozi wa wasafi waliwaalika kesho yake kwenye mkutano na waandishi na kutambua uwepo wao na kupata pia nafasi ya kukutana na msanii mkubwa nchini Nigeria, Wizkid na kupiga naye picha.

“Kwa mfano TID asingetushika mkono siku ya tamasha fursa zote hizi tusingezipata ungekuta tumelala nyumbani, hivyo ndivyo inavyotakiwa wasanii kushikana,”alisema Domokaya.

Kwa mahojiano zaidi kuhusu habari hizi fuatilia kipindi cha MCL Extra siku ya Ijumaa Novemba 15, 2019.

Advertisement