Ni msoto Jos! Gor Mahia vs Homeboyz mashakani

Saturday January 11 2020

Mwanaspoti-Kenya-Tanzania-msoto Jos-Gor Mahia-Homeboyz-MWANASPORT-Michezo leo-mashakani

 

By Fadhili Athumani

Nairobi. Ni ngori budah! Inauma lakini kama anavyopenda kusema Stivo Simple Boy, inabidi tuzoe tu, maana ukweli wa mambo ni kwamba, Ligi kuu ya Kenya imesota sana.

Kukosa mdhamibi kunaumiza vilabu nyingi, mabingwa watetezi, Gor Mahia wakiwemo. Huko Kogalo unaambiwa wachezaji wanalia njaa kinoma Jos!

Ratiba ya KPL, inaonesha kuwa Kogalo wanapaswa kusafiri hadi Bukhungu, mjini Kakamega kuwafuata Kakamega Homeboyz, lakini situation kwa ground ni different mazee. Taarifa iliyoifikia Mwanaspoti ni kwamba, wachezaji hao, wako kwa mgomo baridi, wakidai kukatiwa ganji zao.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mabingwa hao mara 18 wa KPL, ambao hawajafanya mazoezi kuanzia Jumanne, wakishinikiza kulipwa chapaa zao, huku wakiilaumu menejimenti kwa kuwapa ahadi za uongo, bado wamekwama Nairobi, wakati wanatakiwa kuwa wamefika mjini Kakamega kwa ajili ya mechi hiyo muhimu.

"Bado tumekwama Nairobi. Bado tuko gizani maana hakuna mawasiliano yoyote kutoka kwa menejimenti au benchi la ufundi, tunafaa kwenda Kakamega kucheza na Homeboyz, mechi ya Jumapili. Lakini unajua hatuwezi kucheza tukiwa njaa, tunauliza tulipwe hilo tu,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.

Mbali na mechi ya Gor na Homeboyz, kutakuwa na mechi zingine za raundi ya 16 ya KPL, ambapo Tusker FC itaifuata Bandari ugani Mbaraki.

Advertisement

Sofapaka itakutana na Nzoia Sugar, Kisumu All Stars vs Posta Rangers, Chemelil Sugar vs KCB, Ulinzi Stars vs Western Stima, AFC Leopards vs Wazito, huku Mathare United wakiikaribisha Kariobangi Sharks ugani Moi Kasarani.

Advertisement