Karia: Wachezaji kutoingia vyumbani wakati wa mechi ni sawa

Muktasari:

Timu nyingi hasa za Simba na Yanga zimekuwa zikipigwa faini kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa kuhofia vyumba hivyo kupuliziwa dawa.

Dar es Salaam.Licha ya timu kupigwa faini kwa vitendo vya kutoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema ni sawa timu kukaa nje.

Karia ameeleza hayo leo alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa soka nchini katika maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake TFF.

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi ya timu pinzani kupulizia dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, jambo ambalo TFF ilifanya uchunguzi na kubaini tatizo la hewa katika vyumba hivyo si dawa bali ni madirisha madogo.

"Sio uwanja wa Taifa pekee ambapo tumewahi kusikia malalamiko hayo, kuna uwanja Shinyanga ambapo pia ulilalamikiwa na tulipofanya uchuguzi tukabaini hakuna hewa sababu ya madirisha madogo na ni sawa timu kukaa nje kwa kuwa vyumba vya kubadilishia nguo haina hewa," alisema Karia.

Alisema kuhusu baadhi ya timu kushtumiwa kupulizwa dawa hakuna ukweli katika hilo na amesisitiza kuwa mwenye ushahidi juu ya madai hayo alisaidie Shirikisho.

"Sijui ni dawa au uchawi unafanyika, lakini ni maneno ambayo hayana ukweli, hewa nzito katika vyumba ni sababu ya madirisha madogo ndiyo sababu hivi sasa tunashauri dressing room zifungwe AC.