Jon Makini: Muziki Tanzania umejaa ubaguzi

Friday January 10 2020

Mwanaspoti-Jon Makini-Muziki-Tanzania-umejaa-ubaguzi-bongo

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Joh Makini amesema muziki wa Tanzania umejaa ubaguzi na upendeleo wa hali ya juu.

Joh Makini ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Weusi kwa sasa wanatamba na nyimbo Kama Showtime, Wapoloo, Gere, Ni come, Swagire, Ile saa.

Akizungumzia muziki wa Hip Hop Makini alisema muziki umejaa ubaguzi kama ingekuwa kurekodi ndio kufanya vizuri nadhani angekuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo kutoka mkoani Arusha kufanya vizuri kisanaa nchini.

“Wanamuziki wa hip hop hawapewi nafasi inayostahili wanabaniwa wakati muziki wa Bongo Fleva wakipewa nafasi kubwa pamoja na muziki wao kujaa siasa na longo longo tupu,” alisema Joh Makini.

Joh Makini alisema anafanya Hip hip kwa sababu ni muziki pekee alioupenda tangu nikiwa na umri mdogo.

“Ndio maana katika tungo zangu napenda kusisitiza nakotokea ili kufuta dhana ya kuwa wapo wakali na sio Bongo peke yake.”

Advertisement

Joh Makini amewashanga wanamuziki wanaotoka mkoani wakifika jijini Dar es Salaam wanashindwa kutaja sehemu wanayotoka wakiogopa kuonekana washamba.

"Unajua wasanii wengi wanaotoka mkoani wakifika mjini wanakuwa kama wanaona noma kuelezea wanakotokea kutokana ufinyu wa akili zao ambazo huamini kuwa ukisema unatoka mkoa flani utaonekana mshamba na sio mjanja imeshajengeka kuwa mzawa wa Bongo ndio kuwa mjanja” alisema Joh Makini

Advertisement