Diamond: Harmonize, Ali Kiba kushiriki Wasafi Festival -VIDEO

Wednesday October 30 2019

Mwanaspoti-Diamond-Harmonize-AliKiba-kushiriki-Wasafi-Festival-Tanzania-Mwanamuziki-Tamasha-burudani

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond amefungua milango kwa Harmonize na Ali Kiba kushiriki Tamasha la Wasafi Festival Dar es Salaam litakaloanza Novemba 9, 2019 Viwanja vya Posta.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Diamond ambaye ni Mkurugenzi wa Wasafi Media alisema mwanamuziki Harmonize yupo katika orodha ya wanamuziki watakaoshiriki katika tamasha la Wasafi Festival na yupo katika mpango wa kuzungumza na uongozi wa Ali Kiba ili naye ashiriki.

Diamond ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 30, 2019 ikiwa zikiwa zimepita siku chache tangu Harmonize aeleze kutakiwa kuilipa lebo ya wasafi Sh500 milioni ili aweze kuachana nayo na kufanya kazi zake mwenyewe.

Diamond alisema, Harmonize ni mtoto wa nyumbani haiwezekana akakosa kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Dar es Salaam.

"Jamani niwaambie tu Harmonize atakuwepo katika Tamasha la Wasafi Festival, sababu yule ni mtoto wa nyumbani na ana haki yake, na pia hata kaka yangu Ali Kiba nitaongea na uongozi wake ili aweze kushiriki katika Tamasha hili."

Aidha Diamond alisema kutakuwa na mashindano ya madensa ambao kila msanii atakaye kuwa nao wanatuhusiwa kushiriki au makundi tofauti na mshindi akishinda atachukua Sh10 milioni.

Advertisement

Advertisement