Bibi Mwenda azua jambo msiba wa Seth Bosco, azua gari

Monday December 9 2019

Mwanaspoti-Bibi-Mwenda-azua-Tanzania-jambo-msiba-Seth Bosco-azua gari

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam.Mcheza filamu nchini Tanzania, Fatma Makongoro 'Bibi Mwenda' ameanzisha vurugu katika msiba wa Seth Bosco.

Tukio hilo limetokea leo Desemba 9, 2019 muda mfupi kabla ya kuondolewa kwa mwili katika kanisa la KKKT Kimara Temboni ambapo kulifanyika Ibada.

Bibi Mwenda aliyekuwa amevaa gauni la bluu lenye maua na kujitanda mtandio wa rangi ya bluu bahari, alifanya jambo hilo kwa kukaa mbele ya gari maalum lililokuwa limebeba mwili.

Pamoja na watu zaidi ya kumi kumshika ili kumuondoa aligoma na kueleza kuwa atafanya hivyo pindi atakapopewa pesa.

Baadaye alijitokeza mtu na kumpa Sh10,000 ambayo alisema haitishi.

Majibu hayo yalisababisha wanaume wengine watatu kumpa fedha nyingine na hata mmoja ambaye alibakiza Sh1000 mkononi, alimpokonya.

Advertisement

"Hiyo hela na wewe umeiacha ya nini, ilete hapa," alisikika Bibi Mwenda na kisha akamnyanganya.

Msanii Nova aliyekuwepo wakati wa tukio hilo, amesema alichokifabya bibi mwenda ni utani wa makabalia.

"Huu ni utani wao wa makabila, sio unajua huyu mama ni mtani hivyo mpeni tu hela aondoke hapo," amesema Nova.

Advertisement