Beka Flavour: Natamani Yamoto Bendi irudi upya

Wednesday November 20 2019

Mwanaspoti-Beka-Flavour-Natamani-Yamoto-Bendi-irudi-Tanzania-upya-muziki

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Beka Flavour amesema angekuwa na uwezo angeirudisha Yamoto Bendi sasa wangefanya biashara kubwa sababu kila mtu ameshajitengenezea mashabiki wake.

Kundi la Yamoto bend lilikuwa linaundwa na wanamuziki wanne Beka Flevor, Aslay, Maromboso na Enock Bella iliteka soko la muziki wa Tanzania kutokana na uimbaji wao.

Akizungumzia kundi hilo Beka alisema mfano kila mmoja ana mashabiki elfu moja wakichanganya wakifanya shoo watapata faida sababu kila shabiki atataka kuja kumuona msanii wake.

"Baada ya bendi kuvinjika kila moja ameweza kuendesha maisha yake mwenyewe, nakwambia Yamoto Bendi ingekuwepo hadi leo, nahisi tungekuwa 'levo' nyingine, sababu tulikuwa na upepo wa kupendwa na tulikuwa na kichwa kizuri cha kutunga nyimbo nzuri za kuwateka mashabiki,”

“Ningekuwa na uwezo ningeirudisha tungefanya biashara kubwa sababu kila mtu keshajitengenezea mashabiki wake," alisema Beka Flevor

Aidha alisema ndio hivyo haiwezekani kutokana na sasa kila mtu yuko na uongozi wake na haujui amefanyaje hadi amefikishwa hapa. Hata wakitaka shoo ya kuwakusanya itakuwa ngumu kwani kila mmoja ana bajeti yake ya kuchukuliwa.

Advertisement

Beka Flevor anayetamba na nyimbo kama Libebe, Kibenten, Sikinai, Siachani nae, Sarafina alisema tangu ametoka Yamoto bendi maisha yake yamebadirika kwa asilimia kubwa ya kipato na amekuwa tegemezi kwa ndugu na jamaa wanaomzunguka.

Yamoto bendi iliyoanzishwa mwaka 2014 Jijini Dar es Salaam likiwa linaundwa na wasanii Aslay, Beka Flavour, Maromboso na Enock Bella na kuvunjika mwaka 2017.

SABABU YA KUVUNJIKA KWA KUNDI HILI FUATILIA KUSOMA GAZETI LA MWANASPOTI LA IJUMAA

 

Advertisement